Zijue faida kedekede za mlonge
Mlonge ni katika mimea maarufu katika uoto wa kitropiki na nusu tropiki, hujulikana kama radish tree, au kwa kitaalamu zaidi huitwa moringe.
Mmea huu umetunukiwa viambato muhimu kama vitamini Kwa wingi na madini mbalimbali
Majani yake Hutumika pia katika ulimwengu wa mapishi na kona ya tiba mbadala, pia unaweza ukayaandaa kwa kuyakausha kivulini, na kisha kufanya unga, ambao unaweza kutumia katika uji, angalau vijiko viwili kwa kikombe
Pia unaweza kuchemsha majani ya mlonge pasi nakukamua au kuyaunga nazi, kisha ukanywa
Mizizi na maua pamoja na tunda zake pia rasilimali muhimu katika mwili katika kutunza na kuboresha kinga ya mwili. Kula hata tunda tatu kwa siku, na nivema ukatafuna pamoja na karanga au korosho ili kupunguza ukakasi
Maua pia unaweza kupikia katika mboga, mlonge pia katika kona ya mapishi huchanganywa na mboga zengine
Zifuatazo ni faida za mlonge Kwamukhtasali;
1.kuondoa malaria sugu
2.kuongeza kinga ya mwili
3.kupunguza uvimbe
4.kurekebisha sukari ya mwili
5.husaidia kwa wenye shinikizo la damu
Hakuna maoni