• Breaking News

    Jitibu pumu (asthma) kupitia tibambadala

    Pumu au asthma ni katika magonjwa hatari ambayo tiba sahihi kwa wengi imekuwa ni kitendawili, lakini lishe mbadala ni jibu lake, kutokana na tafiti za wataalamu na wadau mbalimbali, tafiti ambazo natija yake ni kupatikana kwa dawa muafaka za ugonjwa huu kupitia vyakula asilia Tumia vitu vifuatavyo kujitibu pumu kupitia tiba mbadala; 1.karafuu,unaweza kuchukua karafuu 5-6,chemsha karafuu ili kupata ujazo wa nusu glasi, kisha ongeza kijiko kikubwa cha asali mbichi, unaweza kunywa asubuhi na wakati wa Kuala. 2.juisi ya limau, tengeneza juisi ya limau, kwa kuchanganya na asali kijiko na mdalasini wa unga, tumia juisi hii murua asubuhi kabla ya mlo na kabla ya Kuala. 3.asali mbichi, na nivema ukachanganya na mdalasini wa unga, na mafuta ya mzaituni kidogo, tumia mchanganyo huu kijiko kimoja mpaka viwili, asubuhi na jioni. 4.kitunguu swaumu (garlic) chukua angalau tembe tano, maji robo lita pamoja na asali mbichi kijiko kikubwa na mdalasini wa unga kijiko. Chemsha pamoja 5.tangawizi,unaweza kuchemsha tangawizi ujazo wa robo lita, weka na kijiko kikubwa cha asali na mafuta ya. Mzaituni kijiko kidogo. 6.kitunguu maji, jitahidi kutumia kitunguu maji kwenye mboga au kachumbali. 7.maziwa,chemsha maziwa ukichanganya na asali kijiko kikubwa na mafuta ya mzaituni kijiko kwakikombe cha maziwa, kunywa yakiwa na moto. 8.binzari ,tumia kiungo hiki kwa wingi (turmeric) katika chakula chako 9.mafuta ya nazi, unaweza kunywa kijiko, au kupikia katika vyakula, kwa sababu kitaalamu mafuta ya nazi yana palmitic acid ambayo humsaidia sana mgonjwa pumu. Pia mgonjwa anashauriwa kula kwa wingi vyakula vifuatavyo : Karoti Mbegu za maboga ,korosho, karanga Vyakula vyenye vitamini C kwa wingi kama matunda Vitu vyenye magniziam kwa wingi kama vitunguu swaumu Maziwa mabichi Mbogamboga kwa wingi Unashauruwa kula nyama nyeupe kama samaki

    Maoni 1 :

    1. Nimefaidika Sana na Elimu hi ya Afya.Naomba masomo haya kuhusu Afya zetu yaendelee....

      JibuFuta

    Post Top Ad

    ad728

    Post Bottom Ad

    ad728