• Breaking News

    Je wajua Siri ilyopo na faida za kuamka asubuhi na Mapema?

    Ndugu yangu mpendwa leo kisiwani tujifnze Siri na faida itikanayo na kuwahi kuamka mapema. Ktk mambo ambayo yanamatokeo chanya na natija kibao ktk afya yako na maisha kwa ujumla ni kuwahi kuamka asubuhi na mapema. Lakini kutokana na ujinga kuchelewa kuamka kumekua ni ufahari na alama ya maisha mazuri. Zingatia; ili kuweza kuamka ktk muda muwafaka jitahidi Kuala mapema. Zifuatazo ni baadhi ya natija zitokanazo na kuamka asubuhi mapema;
    1.husaidia kuzuia uwezekano wakupata ugonjwa wa kukosa kumbukumbu, na kuimarisha afya ya ubongo. haya yanatarajiwa Kwa mwenye Kuala ndani ya masaa muafaka na akaamka mapema.
    2.kuimarisha utendaji kazi wa moyo na mzunguko wa damu, kinyume chake ni kudhoofisha utendaji wake maarufu kwa kitaalamu Kama cardiac functioning.
    3.kupata wasaa mkubwa wa kukamilisha majukumu yako ya kila siku, asubuhi ni kipengele muhimu sana ktk kuyaendea majukumu mbalimbali na kuzidisha ufanisi.
    4.kupata fursa sahihi ya kufanya mazoezi ambayo ni nukta muhimu ktk kuimarisha afya yako
    5.husaidi kupanga ratiba makini na mathubuti ya mizunguko yako ya siku mzima na maisha Kwa ujumla, tafiti za hapa na pale zinaonesha kuwa asubuhi mapema ndio muda pekee ambao ubongo huwa na nguvu na uwezo Wa aina yake.

    Hakuna maoni

    Post Top Ad

    ad728

    Post Bottom Ad

    ad728