Je wajua faida kemkem zitokanazo na matumizi ya asali mbichi?
Ndugu mfuatiliaji wa makala hii, kwanza ni vema kujua kwamba asali tunayozungumzia ni asali mbichi, ndio yenye ufanisi na matokeo chanya ktk afya ya mtumiaji, lakini pia nikutanabaishe kuwa asali ikichanganywa na mdalasini inatoa matunda Mara dufu, zifuatazo ni miongoni mwa faida avunazo mtumiaji wa asali;
1.kuimarisha kinga ya mwili. tambua kwamba asali iliychanganywa na mdalasini, huimarisha mara dufu kinga ya mwili wa mtumiaji, kitahidi kula angalau vijiko viwili vya asali iliyochanganywa na robo kijiko cha mdalasini au habati sauda, fanya hivi kabla ya kulala nauamkapo asubuhi kabla ya mswaki.
2.kupunguza kiasi kikubwa cha lehemu iliyo rundikana mwilini, nayo ni matokeo ya matumizi ya mafuta kupita kiasi ambayo huathiri utendaji kazi wa mifumo ya mwili anuai.
3.kutibu jino, dondoshea mchanganyiko wa kidogo wa asali ulio changanywa na mdalasini na mafuta ya mzaituni ya vuguvugu.
4.Husaidia kuamsha hisia ktk masuala ya jimai, jitahidi kutumia mchanganyiko wa asali na mdalasini, au mchanganyiko wa asali na tangawizi kabla ya kulala au kabla ya jimai
5.....kutibu magonjwa ya ngozi, au kufanya ngozi iwe nyororo, paka eneo husika mchanganyiko wa asali na mdalasini
6..Husaidia kwa wenye tatizo la shinikizo la damu, adumu kutumia mchanganyiko huu wa maajabu
7.kuondoa tatizo la tumbo kujaa gesi, kichefuchefu na kuondoa maumivu ya vidonda vya tumbo, tumia mchanganyiko huu pia
8.kuimarisha harufu nzuri ktk kinywa, sukutua baada ya mswaki kwa mchanganyiko huu wa vuguvugu
9.kuimarisha nywele zako, au ndevu zako, tumia mchangayiko huu maridhawa ,kuoshea nywele na ndevu kadhalika, hukuza haraka na kuimarisha
10.kufuta makovu, kutibu majeraha ya tokanayo na moto,na husaidia kuondoa chunusi zilizo lithium, jipatie tiba masala, rahisi na salama kwa kupitia mchanganyiko huu wa aina yake.
Hakuna maoni