• Breaking News

    Maumuivu ya chini ya kitovu kwa wanawake

    Kwa kitaalamu hujulikana kama lower abdominal
    4
    pain. Tatizo hili limekuwa ni donda ndugu kwa muda na linasumbua wengi katika wanawake .na ugumu huja katika kuliweka wazi tatizo hili ambapo wengi uhisi aibu. Takwimu zinaonesha asilimia kubwa ya wanawake wanasumburiwa na tatizo hili.


    Dalili za tatizo hili huambatana na kusikia maumivu ya  chini ya kitovu wakati wa kuinama, kunyanyua vitu vizito, maumivu katika siku za hedhi tatizo ambalo kitaalamu huitwa Dysmenorrhea au menstrual cramps. Maumivu katika kibofu cha mkojo, wakati wa kucheka, wakati wa Kulala kifudifudi, na wengine huisi maumivu katika tendo la ndoa



    Maumivu haya huweza kuwa chini ya kitovu katikati, au pembeni kulia au kushoto



    Maumivu haya husababishwa na;


    Kuvimba kwa kuta za mji wa mimba (uterus). Pamoja na kuvimba kuta za mirija ya uzazi, tatizo lijulikanalo kama pelvic inflammatory disease



    Pia husababishwa na afya mbovu ya kibofu (bladder) cha mkojo. Kama kusumburiwa na magonjwa ya UTI (urinary tract infection) ambapo bacteria wajulikanao kama E coli hushamburia kibofu cha mkojo na kuzaliana.


    Pia husababishwa na kutokomaa kwa mayai ya uzazi jambo ambalo husababishwa na kuvimba kwa vifuko vya mayai( ovaritis ) na kufanya maumivu mithili ya kichomi.

    Pia husababishwa na mirija ya uzazi kujaa maji mazito na machafu, jambo ambalo hufanya mayai kutotembea vizuri kwenya mirija ya uzazi.


    Namna ya kulikabili tatizo hili kupitia tiba mbadala, ndugu mkeleketwa wa tiba  mbadala nimeona kuwa ipo haja kutokana na ukubwa wa tatizo niorodheshe japo kwa mukhtasari nukta za tibambadala katika kulikabili tatizo kama ifuatavyo;




    Mlonge, ambao hujulikana kitaalam kama moringa oloifera. Unaweza kuandaa unga utokanao na majani ya mlonge. Anika majani ya mlonge kivulini kisha fanya ungaunga. Unga huu wa majani ya mlonge unaweza kutumia kijiko kimoja cha mezani katika uji au supu au juisi ya matunda, vizuri ukatumia mara mbili kwasiku. Mlonge ambao umetunukiwa utajiri wa kalsiam, vitamini kwa wingi husaidia kuondoa tatizo la kuvimba kwa kuta za uzazi.



    Tumia Baking powder, au sodabiki maarufu kama unga wa soda kupunguza maumivu. Baking powder ina antacid property .hii ni kwaajili ya kupunguza maumivu weka nusu kijiko cha baking powder kwenye glasi ya maji yenye vuguvugu. Hii husaidia kunyutrolaizi acidic condition na kuondoa Nairobi.



    Tumia asalimbichi, chukua vijiko viwili vya mezani vya asali pamoja na kijiko cha mdalasini wa unga na maji ya uvuguvugu. Tumia kabla ya Kulala na kabla ya mlo asubuhi.


    Tumia juisi ya limau, tengeneza juisi safi ya limau ,au unaweza kuchukua glasi ya maji ya vuguvugu na kukamulia kipande cha limau. Namna ya kufanya juisi ya limau, changanya katika maji ya limau vijiko viwili vya asali ili kuongeza ufanisi.



    Tangawizi, (ginger) au zanjaabir.matumizi ya tangawizi yanamchango mkubwa sana katika afya yako. Waweza kufanya chai ya tangawizi na kuongeza vijiko kadhaa vya asali na mdalasini wa unga. Huondoa gesi tumboni, kurekebisha mfumo wa mmeng'enyo, kusafisha kibofu.


    Mdalasini. Ni kiungo maarufu katika upwa wa afrika mashariki  na duniani kwa ujumla. Lakini kiungo hiki hakipo nyuma katikaulimwengi wa tibambadala. Unaweza ukautumia kama majani ya chai, au kwa kichanganya na asali mbichi kwa uwiyano wa vijiko viwili vya asali na kijiko kimoja cha mdalasini wa unga .


    Kunywa maji ya kutosha, wastani wa lita tatu kwa kiwango cha chini, maji ya kutosha yanamchango usiosemeka katika kuondosha tatizo hili hususan pale linaposababishwa na matatizo ya kibofu cha mkojo (urinary tract infection).


    Ahsanteni kwa kufuatilia makala hii pendwa.....


    Kwa mawasiliano zaidi na ushauri usisite kuwasiliana nami kwa namba  0782 133015,wako brother Abdulmajiid, MuM, Baed

    Maoni 5 :

    Post Top Ad

    ad728

    Post Bottom Ad

    ad728