Namna ya kuifanya ngozi yako iwe na mvuto na muonekano
Ngozi ni kiungo muhimu Sana katika mwili wa mwanadamu ambapo ipatiwapo matunzo hufanya taswira nzuri na yenye mvuto.
Ngozi hafifu iliyokosa mvuto ni matokeo ya matumizi mabaya ya vipodozi au kushinda juani kwa muda mrefu, kukosa elimu sahihi juu ya matunzo sawiya.
Matumizi ya vyakula na tibambadala yana mchango chanya katika kuboresha kuimarisha na kunawirisha ngozi yako.
Katika makala hii pendwa nimejaribu kuelezea namna ya kuondokana na Mng'aro hafifu, chunusi, makovu sehemu mbalimbali,
Zifuatazo ni namna za kuifanya ngozi yako iwe na muonekano mzuri, halisi na wakuvutia kupitia tiba mbadala;
a). Tumia asali, pakaa asali usoni au sehemu athirika, kisha kaa dakika kadhaa, kisha osha uso wako au sehemu husika kwa kutumia maji ya vuguvugu. Asali husaidia kuhuwisha seli zilizokufa, ni vema ukachanganya na juisi ya limau au maziwa ya unga
b). Juisi ya chungwa, tumia juisi ya chungwa ,vijiko viwili vya mezani pamoja na bizari, jipake usoni kisha kaa baada ya muda ,kisha uoshe na maji ya vuguvugu
c) mshubiri (mualovera), chukua tabaka la juu la mualovera ,yaani lichune kisha tumia kwa kujipaka kisha kaa kidogo kama robo saa, na jioshe kwa kutumia maji ya vuguvugu.
d). Tumia maziwa ya moto. Lakini yawe ya kati na kati. Maziwa yana lactic acid, ambayo husaidia kuhuisha ngozi na kuifanya iwe na mvuto. Hivyo tumia maziwa ya vuguvugu kutwa mara mbili ,takribani Wiki mbili.
e). Tumia papai. Unaweza kutumia papai na uchanganye na juisi ya limau ,jipake eneo husika na utulie dakika 20 ,kisha uoshe uso na maji ya vuguvugu.
f). Kunywa maji ya kutosha. Jitahidi kunywa maji ya kutosha kila siku. Wataalamu wa afya hushauri mtu kunywa maji kwa wingi. Kiwango cha chini kabisa ni lita tatu au nne. Maji yanamchango usioelezeka katika kunawirisha na kuipa mvuto ngozi yako. Maji hufanya mfumo wa taka mwili kuwa katika ubora wake na kuifanya ngozi iwe na unyevu nyevu.
g). Tumia mafuta ya mzaituni (olive oil). Chukua mafuta Ya mzaituni vijiko viwili vya mezani pamoja na asali vijiko viwili, pakaa usoni kwa kutumia kitambaa na kisha subiri dakika 2 mpaka 4 ,halafu osha uso wako au sehemu husika kwa maji ya uvugu vugu, rudia zoezi hili mara mbili kwa siku.
h). Tumia maji ya dafu, pakaa usoni kisha ukae dakika kadhaa, pia unaweza ukanywa maji ya dafu ya kutosha mara kwa mara,. Ndugu mfuatiliaji penda kunya maji ya dafu mara kwa mara ili kuboresha ngozi yako.
I) Tumia matango, kwa jamii zake zote, kama mamung'unya, matikiti maji na mfano wa hayo. Unaweza ukatumia tango kwa kujipaka usoni au sehemu husika kisha kukaa hadi nusu saa na kuosha uso kwa maji ya vuguvugu.
j). Tumia limau, jitahidi kunywa juisi ya limau. Lakini pia kwa ajili ya ngozi unaweza kujipaka maji ya limau kisha kusubiri kama dakika kumi na kujiosha na maji ya moto. Lakini angalizo; usiwe na vidonda usoni, au kupita juani kabla ya kunawa maji.

Hakuna maoni