• Breaking News

    Maajabu ya limau ktk ulimwengu wa tiba mbadala

    Limau ni tunda maarufu, hutumiwa kwa kiasi kikubwa kama kiungo, lakini tambua kuwa limau ni zaidi ya kiungo ktk ulimwengu wa tiba mbadala, tafiti za hivi karibuni Za wadau mbalimbali wa tasnia ya afya zinaonesha kuwa limau lina a
    natija kedekede ktk afya ya mwanadamu .                    Limau limetunukiwa kuwa na viambata muhimu kama vitamini a, b na c kwafujo, pia kuna potasiam, zinki na madini ya chuma pamoja na viambata vinginevyo.
       Limau lli liweze kuleta natija na faidi zaidi ni vema likatumiwa kwa usulubu kama juisi freshi kwa kuchanganywa na asali mbichi na mdalasini wa unga kidogo. Au tengeneza chai safi ya limau, mdalasini na asali. Au limau pekee na maji ya vugu vugu, na chumvi ya mawe.
        Unaweza kutumia juisi hii ya limau kama kifungua kinywa, yaani kabla yachochote, vema iwe ya vuguvugu, pia tumia baada ya mlo kama nusu grassi, kusutua mdomoni, kuoshea nywele na ndevu. kupaka ktk jeraha hasa litokanalo na moto.

        Zifuatazo ni baadhi ya faida zitokanazo na matumizi sahihi ya juisi hii ya limau :

    Husaidia mfumo wa mmeng'enyo wa chakula, na kuongeza ufanisi na utendaji kazi wake, kusafisha tumbo, kupunguza gesi na kuondoa kichefuchefu. Tumia juisi baada ya mlo au weka limau kidogo ktk chakula.

    Husaidia mfumo wa upumuaji, hivyo huwasaidia kwa kiasi fulani wenye pumu, na kuboresha utendaji wa mfumo.

    Husafisha mfumo wa damu mwilini na kuwasaidia wenye tatizo la shinikizo la damu, hivyo mwathirika apendelee kutumia juisi hii.

    Kusafisha figo, na kuondoa uwezekano wa kuwepo vijimawe kwenye figo na kulipa figo lako ufanisi.


    Kuimarisha afya ya nywele na ndevu, kuepuka nywele kukatikakatika,kuondoa mba na kung'arisha nywele zako, osha nywele kwa sabuni kisha kwa maji ya limau.

    Kuondoa matatizo ya meno na vidonda vya kooni na kuimarisha fizi zako, tumia dawa za meno za limau au kusukutua kinywani kwa maji ya limau.

    Kubalanzi kiwango cha sukari mwilini, na kuongeza kinga ya mwili kwa ujumla, kuweka harufu nzuri mdomoni, kuondoa sumu mwilini.











    Hakuna maoni

    Post Top Ad

    ad728

    Post Bottom Ad

    ad728